Vipashio vya Habari:
Home » » AZAM FC WASHINDWA KUTUMIA VYEMA UWANJA WA NYUMBANI

AZAM FC WASHINDWA KUTUMIA VYEMA UWANJA WA NYUMBANI

Written By Ahmada Mwariko on Saturday, April 20, 2013 | 10:52 AM


Timu pekee inayoiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa AZAM FC leo hii imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani kwa kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na timu ya AS Far Rabat kutoka Morocco. Mpambano huo wa kuwania kombe la shirikisho barani Afrika CAF. Mchezo huo ulionekana kuwa na mashambulizi ya zamu huku kila timu ikijaribu kujihami isiweze kufungwa goli, Azam walikosa baadhi ya nafasi nyingi za wazi hali kadhalika wapinzani wao nao walikosa baadhi ya nafasi. Katika dakika ya 65 Kipre Tcheche wa Azam ambaye leo hii alionekana kuwa msumbufu sana katika ngome ya AS RABAT alikosa goli baada ya shuti lake kugonga mwamba na kurudi uwanjani.Azam watakuwa na kazi ya ziada katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa Morocco ambapo wanahitaji sare yoyote ile ya magoli au ushindi ili kuweza kusonga mbele.
Hili ndilo tumaini pekee lililobaki kwa watanzania baada ya timu ya Simba sc kutolewa katika hatua ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa Afrika na FC Deportivo de Liboro.
Kila la kheri Azam
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Jicho La Habari Enhanced by Ahmada Mwariko
Share habari hii kwa wadau :
Like Facebook Page yetu hapa
×
bloggerWidget

FOLLOW ME ON G+

Follow Us On Twitter

UNGANA NASI HAPA

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu Ungana nasi sasa hujachelewa Bonyeza hapo juu, au Sajili email yako hapo chini.

VIEWERS

Don't Forget To Join US Our Community
×
bloggerWidget

Follow Me

Followers

 
Support : Jicho La Habari | Ahmada Mwariko
Proudly powered by Jicho La Habari
Copyright © 2013. jicho la habari - All Rights Reserved
WEB DESIGNER  AHMADA INC
Designed and modified by Ahmada Mwariko